Nilijipata nikiwaza haya.
Hayakuwa ya maana kwenu,
Yalitoweka mithili ya maneno.
Wananchi hawana utulivu,
Kukicha wanapuliza jivu,
Masalio ya wafu na mali,
Najiuliza huu kweli ni uhai?
Heri mfu basi aliyeaga usingizini,
Kuishi na uoga akilini ni hatia,
Kwa nafsi yangu, iliyozoea usalama,
Hawajui nina mipango ya kuhama…
Naitazama ikienda pahala pa upweke,
Inapiga kambi bila furaha,
Wasiwasi anaona haya kumsalimu,
Kwa umbali naiskia harufu ya ndimu.
Kitunguu, kitunguu saumu na mdalasini,
Kuchanganywa pamoja na shubiri,
Nani huyo ananifuata na machungu?
Najitenga wasije wakaninyunyuzia.
Wananitazama waskisubiri nitakacho sema,
Hawapati jibu nafsi yangu ni ya Malaika,
Itakuwaje nijihusishe na wanyama hao?
Wakatali kama wawindaji haramu…
Nazama sasa niwe maji ya mageuzi,
Nijirudishe kwa maumbile ya Mwenyezi,
Ndiposa kila mwezi watafute nafsi yangu,
Watazame juu ninakokaa kama mawingu.
M.O.O aka Carswell evoL